Thursday 6 November 2014

Thursday 10 July 2014

Njia za matunzo ya meno yako


1: KUPIGA MSWAKI:

  • ·      Piga mswaki kwa daikika 2 angalau mara mbili kwa siku.
  • ·      Ni nyema kupiga mswaki kabla ya kulala kwani ulinzi wa meno kwa mate yako ni mdogo ukilinganisha na uwapo macho.
  • ·      Kupiga mswaki baada ya kula ni mazoea mazuri, hukinga uchafu utoknao na chembe za chakula kujijenga kati kati ya meno yako.
  •  

2: KUTUMIA ‘MOUTH WASH’:

  • ·      Tafuta na tumia ‘Mouth Wash’ uipendayo kuyapa nguvu meno yako.
  • ·      Soma maelekezo kan-bla ya matumizi.
  • ·      Wafundishe watoto kati ya miaka 6 -12 jinsi inavyotumiwa  ili wasiimeze.
  • ·      Kumbuka ‘Mouth wash ’ haimezwi.



3: UCHAGUZI WA VYAKULA SAHIHI:

  • ·      Chagua vyakula vyako kwa makini.
  • ·      Epuka kula kula ovyo, jambo linaloongeza uchafu utokanao na vyakula kwenye meno.
  • ·      Epuka vyakula vyenye sukari na vinavyonata, vyakula vya aina hii utengeneza mazingira ya bakteria kuzaliana kwa winigi mdomoni.
  • ·      Pata mlo sahihi (Balance diet ) kwa ulinzi wa meno yako. Mfano ni maji mengi, mboga mboga, matunda, maziwa nk.
  •  

4: KUONANA NA DAKTARI WA MENO:

Jenga tabia ya kuonana na tabibu wa meno angalau mara moja kwa miezi sita na kila uhisapo maumivu ya meno kwa ajili ya utafiti na usafi wa meno yako.


Sunday 27 April 2014

ZICHANE BILA MAUMIVU… JUA LEO!

Huu ni muongozo juu ya kutunza na kuchana nywele asilia bila maumivu au ugumu wowote.
  • Kabla ya kuendelea kusoma; amini kuwa nywele asilia ni rahisi kutunzwa; Unachotakiwa kujua ni JINSI GANI hutunzwa.
  • Pia tambua kuwa; kutokuwepo na masaluni au makala mengi juu ya utunzaji wa nywele asilia hakumaanishi kuwa kuna ugumu katika kutunza nywele hizi bali tu ni uhaba wa watafiti, na unaweza kuwa moja wao. 
  • Nywele zetu ni tofauti na zile za asili ya kizungu, hivyo njia za matunzo na mitindo sio lazima zifanane.

Haya tuendelee; kama nywele nyinginezo, matunzo ya nywele asilia huusisha usafi, michano na mitindo.

1) USAFI 

  • Kwa kutumia shampoo osha nywele zako walau mara moja kwa wiki hata zaidi kama kuna ulazima wa kuondoa mafuta, jasho, vumbi nk. Nywele zenye afya hukua katika mazingira safi. 
  • Kwa kawaida shampoo hukakamaza nywele, hivyo hakikisha watumia kondishina wakati wa kuziosha. Hii hulainisha nywele  na kuzifanya rahisi kuchanwa. 
  • Fanyia stimingi nywele zako mara moja kwa wiki. Kama utainigia katika stima; vaa kofia ya plastiki kabla ya kufanya hivyo kwani joto kali huletea nywele madhara.
  • Wakati wote tumia vidole vyako badala ya kucha kusugua na kumasaji ngozi ya kichwa chako.

TAMBUA: Kuosha nywele hakufupishi nywele kama inavyoaminika; ila tu hurudisha nywele katika asili yake ya kujiviringisha, hivyo achana na imani hii; weka nywele zako safi kwa afya ya nywele zako.

2) JINSI YA KUCHANA NYWELE ASILIA

Inaaminika kuwa nywele asilia ni ngumu na huuma wakati wa kuchanwa; SIO KWELI, ila tu wengi wetu hatujui njia fasaha ya kuchana nywele zetu.

Kabla ya kuendelea, tutambue kuwa kuchana mara kwa mara nywele asilia katika hali ya ukavu hukata nywele.  Hii hutokana na  msuguano pamoja na nguvu itumikayo katika kuvuta nywele iliyojifungafunga wakati wa uchanaji .

Jambo hili hufanya nywele zionekane kama hazirefuki. Ukweli ni kwamba nywele hurefuka muda wote, sema tu mabadiliko hayo hayaonekani kwasababu spidi ya kukatika ni kubwa kuliko ile ya  kurefuka kwa nywele.

NYWELE ASILIA HUCHANWA KATIKA HATUA ZIFUATAZO.

  1. Baada ya kuosha , stimingi nk. Kausha nywele zako kidogo tu kwa kukandamiza taulo juu ya nywele zako kwa sekunde chache. Usikaushe nywele zako kwa kuzipangusa, kwani msuguano kati ya nywele na taulo lako husababisha nywele kukatika .  
  2. Katika nywele zenye unyevu;  paka mafuta yako ya asili (mf zeituni, nazi, jojoba nk) kwenye ngozi.  Mafuta katika hali ya kimiminika ni rahisi kusambaa kama yanapatikana. 
  3. Baada ya hapo sambaza kiasi fulani cha mafuta hayo kwenye kiganja chako kisha yapake juu ya nywele na kwenye ncha zake. Masaji kichwa chako ili kuyasmabaza. 
  4. Kwa kutumia CHANUO LENYE MENO MAKUBWA; anza kuchana nywele zako kuanzia kwenye ncha zake kushuka kwenye ngozi. Kumbuka  kuanza kuchana nywele kuanzia kwenye ngozi kuelekea kwenye ncha  husababisha maumivu makali na hukata nywele kama ncha hizi zimefungamana. 
  5. Baada ya hatua ya 4, ziache nywele zako zikauke kwa hewa. Lakini pia waweza ku-blow-dry nywele zako kuanzia kwenye ncha kuelekea kwenye ngozi; ila tambua kuwa matumizi ya mara kwa mara ya moto huletea nywele madhara.


KUMBUKA: Kila kabla ya kuchana nywele zako , spreyi kiasi fulani cha maji juu ya nywele zako kisha zipake ncha zake kiasi fulani cha mafuta.

Maji na mafuta hulainisha na kuachanisha ncha zilizojifunga hivyo kuwezesha nywele zako kuchanika kirahisi bila maumivu yoyote.

3) MITINDO
  • Furahia mitindo unayoipenda; ila tambua kuwa mitindo salama ni ile isiyokata nywele na hatari ni ile ikatayo nywele. 
  • Ukiona mtindo Fulani unakukatia nywele usijipe moyo; achana nao mara moja, lasivyo utapoteza kiasi kingi cha nywele. 
  • Nywele zenye aftya na zisizokatika hazibaki kwa wingi kwenye chanuo wala bafuni wakati wa kuoshwa. Ukiona hali tofauti na hii jua kwamba kuna tatizo na nywele zako linatotakiwa suluhisho la haraka. 
  • Mfano wa  mtindo hatarishi ni rasta ndogo sana za vitunguu. Mingineyo mingi pia ipo.

                       Tunakutakia makuzi mema ya nywele zako :)



 Kwa maswali na ndondoo zaidi, endelea kufuatilia ukurasa wetu SIRI YA UREMBO pamoja kufanya 
utafiti binafsi.  Wasambazie na warembo wengine.

NATURALS; 6 MONTHS NO DETANGLING!

  • Bored and always feel lazy about detangling your kinky hair? Well here comes a perfect solution for you!
  • FYI: This article is a result of personal Natural hair study for approx. 6 months. It worked well for 4C type I can assume it will do the same for all kind Afro hair.
    Q. Why do we detangle? A. Because our hair tangle!
    Let’s first know how tangling occurs • Tangling happens when the hair TIPS clock together to form knots. • Tangling is at its best on the tips than it is on the rest of hair strands. • If the tips don’t tangle, the rest of the hair is most likely to remain detangled.
    So if you wanna go without detangling, YOU HAVE TO MAKE SURE THAT YOUR HAIR TIPS DOESN’T TANGLE!
    But how?
    You can get a solution for this by answering the following questions:
    1. What products should I use? 2. When should I use them? 3. How should I use them?
    1. WHAT? Beside shampoo and conditioner, LIQUID ORGANIC OIL is of Mega Importance. This kind of oil has an observed effect of maintaining every hair strand separate from each other therefore preventing tangling of the hair.
    • I recommend liquid oil just because it is easy to spread (Time factor is important for me). • Organic oil because, natural hair respond positively to organic oils.
    For easy application, store the oil within the bottle with a spraying top.
    Personally I use normal Olive Cooking Oil for this purpose, and I must say, the result is awesome!!
    2. WHEN? This question is mainly about the time you need to apply the OIL. This is after shampooing, condition and patting your hair a bit dry leaving in some considerable water in the hair. Avoid rubbing your hair when drying cause the friction created increases breakage.
    3. HOW? 1. Divide your hair into 3 parts. Section these parts several times as to apply the liquid oil into the whole scalp.
    2. Now massage the oil in the damp hair to spread it to all parts of your scalp.
    3. Add some more considerable amount of the oil into your palms, and pat it on the hair tips (Very Important) and strands slightly. Spread the oil throughout.
    4. Hold your hair from the tips, stretch it then using a wide comb, comb your hair from the tips running downwards towards the scalp.
    AND THERE YOU ARE! YOUR HAIR WILL NEVER TANGLE… IT’S DONE!!
    NB: Remember to spray some considerable amount of water and add little bit of oil to the tips before combing your hair again.

    LIKE US >>> SIRI YA UREMBO

Thursday 24 April 2014

JE WAPENDA KUWA NA NYWELE ASILIA?

JUA NA KUBALI MAMBO HAYA:

  • Kila aina ya nywele hukua.
  • Nywele hukua ndani ya kipindi fulani cha muda sio ndani ya usiku mmoja.
  • Nywele zako asilia zimejivingirisha , hazijanyooka hivyo KUBALI NA PENDA ASILI YA NYWELE ZAKO.
  • Kama ndivyo, namna ya matunzo na mitindo yake ni tofauti na nywele zilizonyooka.
  • JIAMINI KATIKA MITINDO TOFAUTI NA ILE YA NYWELE ZILIZONYOOKA.





PENDA UKURASA WETU HAPA >> SIRI YA UREMBO :)